KWA CLINICS NA BIASHARA ZA AFYA

Pokea Leads Wengi Bila Kupoteza Hata Mmoja — Hata Ukiwa Umelala.

Pata mfumo unaopokea, kujibu, kuchuja, kufanya follow-up na kukutaarifu pale mteja anapokuwa tayari kununua au kuweka appointment.

✓ WhatsApp 24/7✓ Follow-up ya otomatiki✓ Hot Lead Alerts
KitengoAI Systems Dashboard
Imejengwa kwa biashara zinazopokea leads kupitia Facebook, Instagram na WhatsApp lakini zinapoteza mauzo kwa kuchelewa kujibu, kukosa follow-up na kutokuwa na mfumo wa kusimamia kila mteja.
HILI NDILO TATIZO HALISI

Kila siku unalipia matangazo. Lakini si kila anayekutumia WhatsApp anaishia kuwa mteja.

Wengine wanachelewa kujibiwa. Wengine wanauliza bei halafu wanapotea. Wengine wanahitaji kufuatiliwa kesho, lakini kesho inafika umeanza kushughulika na leads wapya.

Haji Selemani
KUTANA NA MWANZILISHI

“Niliona biashara nyingi za afya hazikosi watu wanaohitaji huduma. Zinakosa mfumo wa kuwahudumia na kuwafuatilia.”

Mimi ni Haji Selemani, mwanzilishi wa KitengoAi.

Kwa zaidi ya miaka 6 nimekuwa ndani ya soko la afya, nikijifunza kwa vitendo jinsi biashara za afya zinavyopata wateja, zinavyotumia matangazo, zinavyojibu WhatsApp, na changamoto zinazozifanya zipoteze mauzo.

Katika kipindi hicho nimegundua jambo moja linalojirudia karibu kila mahali...

Tatizo si kukosa watu wanaohitaji huduma.

Tatizo ni kwamba baada ya watu hao kuwasiliana kupitia WhatsApp:

  • Majibu yanachelewa.
  • Follow-up inasahaulika.
  • Mtu mmoja anabeba mawasiliano yote.
  • Leads wenye nia ya kununua hupotea kimya kimya.

Ndiyo maana nilianzisha KitengoAi.

Sio kuuza AI.

Bali kujenga mifumo inayosaidia biashara za afya kuhudumia leads vizuri, kuokoa muda na kuongeza mauzo kupitia WhatsApp AI Sales Systems.

Kwa nini nilijenga KitengoAi?

✓ Ili hakuna lead anayepotea kwa kuchelewa kujibiwa.
✓ Ili follow-up isitegemee kumbukumbu ya mtu mmoja.
✓ Ili mmiliki wa biashara arudishiwe muda wa kuendesha biashara.
✓ Ili matangazo yawe na nafasi kubwa ya kubadilika kuwa mauzo.
01

Leads wanaingia, lakini mauzo hayalingani

Bila mfumo wa kuwachuja na kuwaongoza, wengi wanaishia kwenye mazungumzo yasiyofunga mauzo.

02

Mtu mmoja anabeba kila kitu

Anajibu, anafuatilia, anahifadhi taarifa na bado anafanya kazi nyingine. Akizidiwa, leads huanza kupotea.

03

Follow-up inasahaulika

Mteja hakuwa tayari leo, lakini angeweza kuwa tayari baada ya siku mbili. Bila mfumo, mawasiliano yanaishia hapo.

04

Hujui nani yuko tayari kununua

Hot, warm na cold leads wanachanganyika. Muda wako unaishia kwa watu wasio tayari kuchukua hatua.

TATIZO SI MATANGAZO PEKEE

Unaweza kuongeza budget ya matangazo na bado ukaendelea kupoteza pesa.

Tangazo linaweza kuleta watu wengi. Lakini kama hakuna mfumo wa kuwapokea, kuwajibu, kuwachuja na kuwafuatilia, ongezeko la leads linaweza kuongeza mzigo badala ya kuongeza mauzo.

Tatizo halisi mara nyingi si kukosa watu wanaohitaji huduma zako. Tatizo ni kukosa mfumo wa kuwabadilisha kutoka maulizo kwenda appointment, oda au malipo.

SULUHISHO

Kutana na AI Sales System

Huu si mfumo wa kujibu “Habari” pekee. Unafundishwa kuhusu biashara yako, huduma zako, maswali ya wateja na namna unavyotaka mchakato wa mauzo uendeshwe.

Unafanya kazi kama msaidizi wa mauzo wa saa 24 anayepokea kila lead, kufanya mahojiano ya msingi, kuhifadhi taarifa, kufanya follow-up na kukuita pale mteja anapokuwa tayari kuchukua hatua.

Anajibu kwa haraka
Hata usiku, ukiwa na mgonjwa au ukiwa nje ya ofisi.

Anachuja leads
Anatambua anayehitaji huduma, anayefikiria na ambaye bado hajawa tayari.

Anafanya follow-up
Hawasahauliki wale ambao hawakununua siku ya kwanza.

Anakupa taarifa
Unajua nani yuko tayari kuwekewa appointment au kufungwa mauzo.

MFUMO UNAFANYAJE KAZI?

Kutoka kwenye tangazo hadi kwenye mauzo — bila lead kupotea njiani.

1

Tangazo

Mteja anaona tangazo Facebook au Instagram.

2

WhatsApp

Anatuma ujumbe na anapokelewa mara moja.

3

Qualification

Mfumo unauliza maswali muhimu hatua kwa hatua.

4

Majibu

Anapata maelezo yanayolingana na hitaji lake.

5

CRM

Taarifa zake zinahifadhiwa kwa mpangilio.

6

Follow-up

Mfumo unamfuatilia bila kusahau.

7

Lead Score

Anatambuliwa kama Hot, Warm au Cold.

8

Notification

Unataarifiwa pale anapokuwa tayari.

9

Appointment

Lead anaelekezwa kuweka appointment au kuagiza.

10

Close

Wewe unaingia pale thamani yako inahitajika zaidi.

MATOKEO UNAYONUNUA

Baada ya kuwa na mfumo huu utaweza...

Kujibu leads 24/7

Hakuna anayelazimika kusubiri mpaka asubuhi ili kupata jibu la kwanza.

Kupunguza leads wanaopotea

Kila lead anapokelewa, anahifadhiwa na anafuatiliwa kwa mpangilio.

Kuongeza appointments

Leads walio tayari wanaongozwa kuchukua hatua badala ya kuishia kuuliza tu.

Kuokoa muda

Maswali yanayojirudia na mahojiano ya msingi yanafanywa bila wewe kukaa kwenye simu muda wote.

Kujua Hot Leads

Unatumia muda wako kwa watu wenye uwezekano mkubwa wa kununua.

Kupima biashara yako

Unaona taarifa za leads, hatua walizofikia na maeneo yanayohitaji maboresho.

FIKIRIA HALI HII

Unaamka asubuhi na mfumo tayari umefanya kazi kabla hujafungua simu.

Leads walioingia usiku wamejibiwa.

Taarifa zao zimehifadhiwa.

Wale wenye interest kubwa wametambuliwa.

Wengine wamewekewa follow-up.

Na wewe umepewa taarifa ya watu wanaohitaji attention yako.

Badala ya kuanza siku kwa kujibu kila mtu kutoka mwanzo, unaanza kwa kuchukua hatua zinazoweza kuleta mauzo.

TOFAUTI INAONEKANA HAPA

Biashara inayotegemea mtu mmoja dhidi ya biashara yenye mfumo.

EneoBila MfumoNa AI Sales System
Muda wa kujibuHutegemea upatikanaji wa mtuMajibu 24/7
Follow-upHusahau au hufanywa kwa kuchelewaHufanywa kwa mpangilio
Taarifa za leadZimetawanyika kwenye chatsZinahifadhiwa kwenye CRM
Hot leadsNi vigumu kuwatambuaWanapewa kipaumbele
UkuajiLeads wengi huongeza mzigoMfumo unasimamia volume kubwa
SI CHATBOT YA KAWAIDA

Chatbot hufuata majibu yaliyowekwa. AI Sales System huelewa muktadha wa mazungumzo.

Chatbot ya kawaida inaweza kutoa menu au jibu lilelile kila mara. AI Sales System inafundishwa kuelewa huduma zako, kuuliza swali linalofuata kulingana na jibu la mteja na kutambua hatua aliyofikia.

AI Sales System inaweza:

✓ Kufanya mahojiano ya msingi

✓ Kutumia majibu ya mteja kuamua swali linalofuata

✓ Kutambua interest na readiness

✓ Kuhifadhi taarifa muhimu

✓ Kutoa handover kwa mtu halisi inapohitajika

ROI YA MFUMO

Huhitaji kuokoa kila lead ili mfumo ujilipe.

Angalia thamani ya mteja mmoja katika biashara yako. Kisha hesabu ni leads wangapi unapoteza kwa kuchelewa kujibu au kukosa follow-up.

Mfano:
Ukipokea leads 300 kwa mwezi, na mfumo ukasaidia kurejesha wateja 5 tu ambao walikuwa wapotee, thamani yake inaweza kuzidi gharama ya mfumo kulingana na faida ya kila mteja.

Matokeo hutofautiana kulingana na offer, bei, ubora wa leads, huduma na namna biashara inavyofunga mauzo. Mfumo si dhamana ya kiwango maalumu cha mapato.

Jiulize maswali haya:

1. Lead mmoja anayekuwa mteja ana thamani gani?

2. Unapoteza leads wangapi kwa mwezi?

3. Ni mauzo mangapi yanachelewa kwa kukosa follow-up?

4. Muda wako wa kujibu maulizo una thamani gani?

Gharama kubwa si kununua mfumo. Gharama kubwa inaweza kuwa kuendelea kupoteza leads bila kujua.

BIASHARA HALISI ZINAZOTUMIA MFUMO

Huhitaji followers wengi ili mfumo ukusaidie kuongeza mauzo.

Kilicho muhimu si ukubwa wa account yako pekee. Kilicho muhimu ni namna unavyopokea, kujibu, kuchuja na kufuatilia watu wanaokuja kupitia matangazo na WhatsApp.

ShlemCare PreshaFit Instagram account
ShlemCare HerbsHealth

Followers wachache, lakini mfumo na matangazo vilisaidia kuongeza mauzo.

ShlemCare ni mfano kwamba biashara haihitaji kuwa na followers makumi ya maelfu kabla ya kujenga mfumo. Leads wanapopatikana, kinachofuata ni kuwajibu haraka, kuwachuja na kuwafuatilia kwa mpangilio.

Eddos Natural Products Instagram account
Eddos Natural Products31K+ Followers

Account kubwa inahitaji mfumo unaoweza kushughulikia volume kubwa ya maulizo.

Mfumo unasaidia kupokea mawasiliano, kufanya qualification, kuhifadhi taarifa na kupunguza utegemezi wa mtu mmoja kujibu kila lead kwa mikono.

Shansule Fertility Instagram account
Shansule Fertility10K+ Followers

Kwa huduma zenye mahojiano mengi, mfumo husaidia qualification mapema.

AI Sales System inaweza kuuliza maswali ya msingi, kuelewa hitaji la lead, kufanya follow-up na kuhamisha mazungumzo kwa mtu halisi pale inapohitajika.

Una followers 500, 5,000 au 50,000? Mfumo hauanzi na followers. Unaanza na kila lead anayekutumia ujumbe.

Kama tayari kuna watu wanaokuja kupitia Facebook, Instagram au WhatsApp, unaweza kuanza kuweka mfumo wa kuwahudumia vizuri. Na kama unapanga kuongeza matangazo, ni bora kujenga mfumo kabla volume haijawa kubwa kuliko uwezo wako wa kujibu.

PILOT PROGRAM

Anza na mfumo uliotengenezwa kulingana na biashara yako.

Pilot Program inakupa nafasi ya kujenga, kufundisha na kuanza kutumia mfumo kwenye biashara yako kabla ya kuingia kwenye usimamizi wa kila mwezi.

Dirisha la sasa la Pilot Program linafungwa baada ya:

Muda uliobaki wa kujiunga kwenye dirisha la sasa la Pilot Program.

00SAA
00DAKIKA
00SEKUNDE

Kwa nini kuna urgency? Kila mfumo unahitaji onboarding, kuingiza taarifa za biashara, majaribio na marekebisho. Hivyo setups hupokelewa kwa idadi inayoweza kusimamiwa vizuri.

PILOT OFFER THAMANI YA MFUMO: TZS 500,000–800,000

Thamani ya kawaida TZS 500,000 hadi 800,000

TZS 350,000

Ofa ya sasa ya kujenga na kuanzisha mfumo wako.

  • 1. Kuchambua biashara na kupanga sales flow
    Tunaelewa huduma zako, aina ya wateja, maswali wanayouliza na hatua wanazopitia kabla ya kununua.
  • 2. Kujenga AI Sales System yako
    Mfumo unatengenezwa kulingana na biashara yako, si template ya biashara zote.
  • 3. Kufundisha mfumo kuhusu biashara yako
    Tunaingiza huduma, offer, bei, maswali ya kawaida, qualification rules na namna ya kuzungumza na wateja wako.
  • 4. Kuunganisha WhatsApp, CRM na taarifa za leads
    Leads wanapokelewa, taarifa zao zinahifadhiwa na hatua walizofikia zinaonekana kwa mpangilio.
  • 5. Kujenga follow-up, lead scoring na notifications
    Mfumo unatambua Hot, Warm na Cold leads, kufanya follow-up na kukutaarifu pale mtu anapokuwa tayari.
  • 6. Testing, marekebisho, onboarding na support
    Tunapima mazungumzo, kurekebisha flow, kukufundisha kutumia mfumo na kutoa support wakati wa kuanza.
Baada ya Pilot:
TZS 150,000 kwa mwezi kwa hosting, matumizi ya mfumo, maintenance, monitoring na support. Gharama maalumu za matumizi ya AI/API zinaweza kutegemea volume ya mawasiliano na zitaelezwa wakati wa onboarding.
NATAKA KUONA DEMO

Usilipe kabla ya kuona demo na kuthibitisha kuwa mfumo unaendana na biashara yako.

SETUP GUARANTEE

Tutarekebisha mfumo mpaka flow iliyokubaliwa ifanye kazi kama ilivyoainishwa.

Kabla ya kuanza, tunakubaliana kuhusu kazi ambazo mfumo utatekeleza. Ikiwa baada ya setup kuna sehemu ya flow iliyokubaliwa haifanyi kazi kwa sababu ya utekelezaji wetu, tutafanya marekebisho ndani ya kipindi cha Pilot bila malipo ya ziada.

Guarantee hii inahusu utendaji wa mfumo uliokubaliwa, si dhamana ya idadi maalumu ya mauzo, appointments au mapato. Matokeo ya biashara hutegemea pia offer, bei, traffic, ubora wa leads na closing.

NANI ANASTAHILI?

Mfumo huu unafaa zaidi kama...

✓ Unapokea leads kutoka matangazo au organic content.

✓ WhatsApp ndiyo njia kuu ya mawasiliano na wateja.

✓ Unapoteza leads kwa kuchelewa kujibu au kukosa follow-up.

✓ Unataka kuongeza appointments, oda au sales conversations.

✓ Uko tayari kutoa taarifa sahihi za huduma zako ili mfumo ufundishwe.

Haufai sana kama...

✕ Huna offer iliyoeleweka.

✕ Hupati leads kabisa na hutaki kuanza marketing.

✕ Unataka mfumo utoe ahadi za tiba au taarifa zisizo sahihi.

✕ Unatarajia AI ifunge kila mauzo bila ushiriki wa biashara.

MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA

Kabla hujaomba demo, haya ndiyo unapaswa kujua.

1. AI Sales System ni chatbot?

Hapana. Inaweza kuwa na sehemu za chatbot, lakini mfumo mzima unahusisha qualification, CRM, follow-up, lead scoring, notifications na handover kwa mtu halisi.

2. Inafanya kazi kwenye WhatsApp Business?

Inatumia WhatsApp Cloud API. Namba, Meta Business setup na mahitaji ya technical yatahakikiwa wakati wa onboarding.

3. Mfumo unaweza kujibu saa 24?

Ndiyo, ukiwa online na integrations zake zikiwa active, unaweza kupokea na kujibu leads muda wote.

4. Mfumo utajua huduma zangu?

Ndiyo. Tunaundaa kwa kutumia taarifa, maswali ya kawaida, offer, process na masharti ya biashara yako.

5. Unaweza kuweka appointment?

Ndiyo, flow inaweza kuelekeza appointment, kukusanya tarehe inayopendekezwa au kuunganisha na mfumo wa booking kulingana na setup.

6. Follow-up inafanyikaje?

Ratiba na ujumbe huwekwa kulingana na hatua ya lead, kwa mfano baada ya siku 1, 3, 7 au ratiba nyingine inayofaa biashara yako.

7. Nitajuaje Hot Lead?

Mfumo hutumia majibu na tabia ya lead kutambua interest na readiness, kisha hutuma notification au kuweka status kwenye CRM.

8. Mfumo unaweza kufanya makosa?

Ndiyo, AI si kamili. Ndiyo maana tunafanya testing, kuweka guardrails na kuhamisha mazungumzo kwa mtu halisi pale inapohitajika.

9. Gharama ya Pilot ni kiasi gani?

Ofa ya sasa ya kujenga na kuanzisha mfumo ni TZS 350,000. Thamani ya kawaida ya kazi hii ni kati ya TZS 500,000 na 800,000 kulingana na ukubwa na mahitaji ya biashara.

10. Subscription ni kiasi gani?

Baada ya Pilot, subscription ni TZS 150,000 kwa mwezi kwa hosting, maintenance, monitoring na support. Matumizi makubwa ya AI/API yanaweza kuwa na gharama kulingana na volume.

11. Kuna guarantee ya mauzo?

Hapana. Tunatoa guarantee ya kurekebisha flow iliyokubaliwa ili ifanye kazi kama ilivyoainishwa, lakini hatudhamini kiasi maalumu cha mauzo.

12. Inachukua nafasi ya wafanyakazi?

Lengo ni kupunguza kazi zinazojirudia na kuwasaidia wafanyakazi waingilie kwenye mazungumzo muhimu zaidi, si lazima kuwaondoa.

13. Data za wateja zinahifadhiwa wapi?

Inaweza kuhifadhiwa kwenye Google Sheets au CRM iliyokubaliwa. Access na utunzaji wake huwekwa kulingana na setup ya biashara.

14. Naweza kuona demo kabla ya kulipa?

Ndiyo. CTA zote kwenye ukurasa huu zinakupeleka kuomba demo kwanza.

15. Nianzie wapi?

Bonyeza “Nataka Kuona Demo,” eleza aina ya biashara yako, idadi ya leads na changamoto kubwa ya WhatsApp. Kisha utaelekezwa hatua inayofuata.

HATUA INAYOFUATA

Usiongeze leads kabla hujawa na mfumo wa kuwahudumia.

Ona AI Sales System ikifanya kazi. Kisha tutaangalia kama inaweza kuendana na clinic, pharmacy, herbal clinic, wellness center au biashara yako ya afya.

NATAKA KUONA DEMO

WhatsApp: 0632 676 664

WhatsApp Demo